Matumizi ya mbinu za lugha katika kuendeleza maudhui mfano katika tamthilia za kiswahili mizigo na kimya kimyakimya.
Abstract
Lengo kuu la utafiti huu lilikuwa kuchunguza namna Matumizi ya mbini za lugha katika kuendeleza maudhui mfano katika tamthilia za Mizigo na Kimya Kimya Kimya Pia, malengo mahususi yalikuwa mawili; ambayo ni; Kuchunguza maudhui yanayojitokeza katika tamthilia ya Mizigo na Kimya Kimya Kimya na Kubainisha mbinu za lugha katika tamthilia ya Mizigo na Kimya Kimya Kimya na Kuonyesha jinsi mbinu za lugha zinavyoendeleza maudhui katika tamthilia ya Mizigo na Kimya . Utafiti huu ulikuwa ni utafiti wa maktabani na ulifanyika katika jiji la Kampala. Kampala iliteuliwa kwa sababu ndipo mahali ambapo maktaba zenye vitabu mbalimbali zinapopatikana ikilinganishwa na sehemu nyingine yoyote. Maktaba ya Chuo Kikuu cha Makerere ilitumiwa. Matokeo ya utafiti ni kwamba tamthilia ya Mizigo na Kimya Kimya Kimya zinavyolingana na kutofautian na mbinu za lugha ambazo zilitumika.