Show simple item record

dc.contributor.authorAtholere, Vick
dc.date.accessioned2021-05-17T13:34:34Z
dc.date.available2021-05-17T13:34:34Z
dc.date.issued2021-05-14
dc.identifier.citationAtholere,V. (2021).Chanzo cha makosa ya kitahajia katika uandishi wa insha za Kiswahili miongoni mwa insha za wanafunzi wa shule za upili wakidato cha tatu na nne wilayani Kaseses. Unpublished undergraduate dissertation. Makerere University; Kampala-Uganda.en_US
dc.identifier.urihttp://hdl.handle.net/20.500.12281/10740
dc.descriptionA Dissertation submitted in partial fulfilment of the requirements for the a Ward of a Degree of Bachelor of Arts with Education of Makerere University.en_US
dc.description.abstractUtafiti huu ulikusudia kuchunguza chanzo cha makosa ya kitahajia katika uandishi wa insha za Kiswahili miongoni mwa insha za wanafunzi wa shule za upili kidato cha tatu na nne wilayani Kasese. Lengo kuu la utafiti lilikuwa ni kuchunguza chanzo makosa yanayofanywa katika insha za Kiswahili kwa wanafunzi wa shule za upili wailayani Kasese na madhumuni mahususi yalikuwa ni kubaini makosa ya wanafunzi wanayofanya wakati wa kujifunza insha za Kiswahili katika shule za upili wilayani Kasese, kutathmini athari za makosa yanayofanywa katika insha za Kiswahili wilayani Kasese hasa wanafunzi wa kidato cha tatu na nne, na kutambua njia ambazo zinaweza kutumiwa ili kupunguza makosa yanayofanywa na miongoni mwa wanafunzi wanaojifunza lugha ya Kiswahili hasa wakati wa kuandika insha. Utafiti huu pia ulikuwa na maswali kama Je, ni makosa gani yanayofanywa wakati wa kuandiaka lugha ya Kiswahili hasa katika insha za Kiswahili?, ni, athari zipi za makosa yanayofanywa katika insha za Kiswahili kwa wanafunzi wanaojifunza insha za Kiswahili wilayani Kasese? na ni njia zipi ambazo zinaweza kutumiwa ili kupunguza makosa yanayofanwa na miongoni mwa wanafunzi wanaojifunza insha za Kiswahili wilayani Kasese? Utafiti huu ulikuwa na umuhimu wa kumsaidia mtafiti kutimiza baadhi ya mahitaji ya kuhitimu shahada ya sanaa na elimu ya Chuo Kikuu cha Makerere, kumsaidia mtafiti kutambua makosa yanayofanwa na miongoni mwa wanafunzi katika kujifunza insha za Kiswahili na marejeleo ya utafiti huu yatakuwa kama kukumbukumbu katika kitivo cha elimu katika chuo kikuu cha Makerere na kwa watafiti wengine. Utafiti huu ulifanyiwa katika wilaya ya Kasese na katika mjini wa Kasese ambapo shule ya upili ya Kasese, Kilembe na Rwenzori zinapatikana. Mbinu tatu za ukusanyaji data zilitumiwa ambazo ni hojaji, mahojiano na uchunguzi shirikishi. Utafiti huu uligunduwa chanzo cha makosa ya kitahajia katika uandishi wa insha za Kiswahili ni lugha mama, mazingira wanamotoka wanafunzi na ufundishaji duni wa lugha ya Kiswahili. Vile vile, mtafiti aligundua kuwa makosa hayo ya kitahajia yanawaathiri wanafunzi na husababisha wanafunzi hao kufeli na kuanguka mitihani mwishoni mwa mulula na matokeo huwa mabaya. Utafiti huu ulitoa hitimisho kwamba serikali ifanye Kiswahili kuwa lugha ya rasmi ili wanafunzi wawe na uzoefu wa kukizungumza ili wakifika kiwango cha kuandika insha wawe hawana utata wowote.en_US
dc.language.isootheren_US
dc.publisherMakerere University.en_US
dc.titleChanzo cha makosa ya kitahajia katika uandishi wa insha za Kiswahili miongoni mwa insha za wanafunzi wa shule za upili wakidato cha tatu na nne wilayani Kaseses.en_US
dc.typeThesisen_US


Files in this item

Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record