Mikondo ya maudhui kwenye tamthilia teule za Kiswahili zenye mandhari ya ukoloni
Abstract
Kazi hii ninaitabarukia wazazi wangu, familia yangu na watu wengine kwa msaada walionipa katika safari yangu ya kufanya utafiti huu. iv Kwanza, ninamshukura sana Mwenyezi Mungu kwa kunijalia uzima na uwezo wa kukamilisha utafiti huu. Pasipo Rehema zake singeweza kukamilisha kazi hii nzito. Pili, ninamshukuru sana Bw. Nsereko Nelson wa Chuo Kikuu cha Makerere aliyekubali kuwa msimamizi wangu katika kazi hii. Hakuchoka kunitia moyo katika kipindi chote cha kazi hii. Ningependa kuwashukuru pia wahadhiri wangu wasomo la Kiswahili vote wa chuo Kikuu cha Makerere hasa Bw. Nsereko Nelson, Dkt Asiimwe Caroline, Bw. Kyomuhendo Victor, Bw. Wambete Francis, Bw. Ndyanabo Emmanuel, Dkt Jjingo Caesar na Dkt Masengo Innocent. Pia, shukrani zangu ziwaendee watafitiwa vote ambao walikubali kushiriki katika utafiti huu na kutoa data zilizotumika. Naishia nikiwashukuru wengine vote waliosaidia kwa namma moja au nyingine katika kufanikisha kukamilika kwa utafiti huu ambao hawako katika makundi tajwa hapo juu.