Nafasi ya methali na misemo katika ujenzi wa maudhui katika tamthilia za kiswahili; mfano wa tamthilia za mzalendo kimathi na kilio cha haki
Abstract
Utafiti huu unahusu Nafasi ya methali na misemo katika ujenzi wa maudhui katika tamthilia za kiswahili; mfano wa tamthilia za mzalendo kimathi na kilio cha haki. Lengo kuu la Utafiti huu ni kunachunguza nafasi ya misemo na methali kwa kujenga maudhui katika tamthilia za kiswahili kwa kutumia mfano wa Mzalendo kimathi na Kilio cha haki. Katika kufika lengo la utafiti huu, nimetumia nadharia ya kimaadili na nadharia ya elimu mtindo kwa lengo la kuchambua methali na misemo na maudhui zinzazo yajenga Nimegunduwa kwamba wandishi wa tamthilia hizi mbili yaani mzalendo kimathi na kilio cha haki walutumia mesemo na methalj katika kujenga maudhui mbali mbali na pia kuboresha kazi zao za kifasihi. Tukiona mfano moja ni kutoka katika kilio cha haki ambapo Mwandishi Alamin Mazrui ametumia methali ya dalili ya mvua ni mawingu ili kujenga maudhui ya utamaduni na
siasa katika tamthilia hiyo ya kilio cha haki. Katika tamthilia ya mzalendo kimathi tunamuona mwandishi Ngugi wa thiongo na Micere Mugo wakitumia msemo wa Haki ni nguvu kujenga mudhui ya ukoloni, Uzalendo na pia ushuja yaani Herseson Anamuelezea Kimathi kwamba hata yeye hange kubali haki yake ichukuliwe na atafanya kila liwekanalo kizitetea gaki zake kama Mkenya kwasababu ameishi Nyeri kwa mda mrefu. Najwahivyo, ili kukamilisha malengo ya utafiti huu,, data za utafiti zilikusanywa kwa kutumia mbinu ya usomaji wa machapisho. Matokeo ya utafiti huu yanaonesha kwamba Waandishi wa
Tamthilua wana tumia fani kadha kujenga maudhui yao na fani zilizozingatiwa katika utafiti huu zilikuwa misemo na methali. Utafiti huu umeonyesha vile vipengele vya fani yaani methali na misemo vilivyo tumiwa kujenga maudhui. Kwa hivyo, ninahitimisha kwamba methali na misemo zina nafasi kubwa katika kujenga maudhui katika tamthilia za kiswahili