Athari za lugha ya Kinyankole katika ufundishaji wa Lugha ya Kiswahili.
Abstract
Lengo kuu la utafiti huu ni jinsi ambavyo mtoto wa kinyankole anayefunza lugha ya kiswahili anavyoathiriwa na lugha take ya mama katika harakati sake za kujifunza lugha ya kiswahili sanifu. Utafiti huu umefanywa katika wilayani Ibanda. Taasis moja ilishikishwa shule ya upili ya ibanda. Utafiti huu umetumia mbinu ya dodoso, hojaji na mahojiano ya makundi katika
ukusanyaji wa data. Matokeo ya utafiti huu umebaini kwamba pana athari za lugha ya kinyankole katika kujifunza lugha ya Kiswahili sanifu. Hii inatokana na sababu ya watoto kuhamisha uelewa wa lugha ya pili ambayo ni lugha ya kiswahili. Watoto walii wengi wana athari ya lugha ya mama. Mapendekezo yangu ni kwamba lugha ya kinyankole inaleta athari kwa watoto wa kinyankole na wanyankole wenyewe wanapokuwa wanajifunza lugha ya kiswahili. Kwa hivyo pana haja ya kuanza kujifunza lugha hii ya Kiswahili katika mazingira ya nyumbani ili awe nauwezo wa kutumia kiswahili sanifu. Mtoto wa kinyankole akijifunza lugha
ya kiswahili yangu utotoni kutamwezesha kuimudu lugha hii ya kiswahili sanifu na hivyo kumsaidia kumdu somo la kiswahili shuleni pamoja na masomo mengine bila ya kuwa na usumbufu katika maendeleo yake kitaaluma ikizingatiwa kwamba takribani karibu shule zote za secondarily na za msingi za serikali nchini wanafunzi hufundishwa kwa kutumia lugha hii ya kiswahili sanifu isipokuwa somo LA kiingereza. Hivyo kwa mtoto wa kinyankole kuimudu lugha hii ya kiswahili sanifu yangu utotoni ni hatua mojawapo muhimu katika maendeleo yake shuleni.