Usawiri wa wanaume katika nyimbo za mapenzi za kiswahili
Abstract
Andiko hili la mradi linalenga kuchunguza usawiri wa wanaume katika nyimbo za mapenzi za kiswahili.
Mradi huu unalenga kugundua namna wanaume wanavyooneshwa katika nyimbo hizi za kiswahili kama
vile mapenzi, mapenzi hisia na nambari moja. Lengo la mradi huu limeshughulikiwa ipasavyo baada ya
kukusanya data za mradi kwa kutumia mbinu za usomaji makini na upitiaji wa nyaraka. Matokeo ya radi yamebainishwa kuwa mwanaume amesawiriwa kwa nafasi mbili yaani chanya na hasi kama vile;
Mwenye mapenzi, anajali, mwenye madharau, jasiri, mtiifu, mwadilifu, mvumilivu, na kadhalika.