Matumizi ya lugha ya upole na ukarimu katika ndoa za Waswahili na Watooro
Abstract
Utafiti huu utahusu mada ambayo ni matumizi ya lugha ya upole na ukarimu katika ndoa za waswahili na watooro. Ni vizuri kuelewa kwamba kila jamii ina hadithi kuhusu jinsi lugha yake ilivyozuka na matumizi ya lugha hiyo. Lugha imewahi kufafanuliwa kwa jumla kama mfumo wa sauti za nasibu za kusemwa zinazotumiwa na watu wa jamii Fulani wenye utamaduni unaofanana kwa madhumuni ya mawasiliano katika jami hiyo.