Usawiri wa mwanamke kama kiumbe anayejikwamisha kiukombozi kwa kurejelea ya riwaya ya nyota ya Rehema na Utengano
Abstract
Utafiti huu ulichunguza usawiri wa mwanamke kama kiumbe anayejikwamisha mwenyewe katika riwaya ya Utengano iliyoandikwa mwaka wa 1980 na mwandishi Said A Mohammed ambaye ni professor wa taaluma za fasihi na riwaya ya Nyota ya rehema iliyoandikwa na Mohammed Suleiman mohammed mwakani 1972 katika pwani Zanzibar nchini Tanzania.
Mwanamke ni mwanadamu wa jinsia ya kike kwa maana anafaa kuwa mke. Ndiyo sababu kwa kawaida anaitwa hivyo aliyefikia utu uzima. Kabla ya hapo huwa anaitwa mtoto wa kike, binti, mwanamwali au msichana. Baada ya kuzaa anaitwa maama kwa
kawaida jina lenye heshima kubwa katika utamaduni wa aina nyingi. Akianza kupata wajukuu anajulikana kama bibi au nyanya. Wanawake ni takribani nusu ya watu wote duniani.
Wanawake katika riwaya ya utengano ni kama Bi. Tamima na binti yake Maimuna, kazija ambaye ni mhusika Malaya katika riwaya, Bi. Farashuu ambaye ni mkunga na Biti Kocho. Katika riwaya ya Nyota ya Rehema, wanawake ni mithili ya Rehema mwenyewe, Bi. Adilla, Bi. Aziza, Chiku, Ruzuna na Kidawa
Kwa ujumla, wasomi hawa wametoa mchango mkubwa katika kumueleza mwanamke katika hali ya tabia, juhudi zake mafanikio na changamoto au vikwazo hivyo. Baadhi ya tafiti hizi ni pamoja na hizi zifuatazo.