Kulinganisha mtindo wa methali za Kiswahili na za Kikiga.
Abstract
Utafiti huu unalenga kulinganisha mtindo wa methali za Kiswahili na za Kikiga. Utafiti huu ulikua na malengo kama yafuatayo; Lengo kuu la utafiti ni kulinganisha mtindo wa methali za Kiswahili na za Kikiga. Malengo mahususi ni; Kujadili mtindo wa methali za Kiswahuli, Kujadili mtindo wa methali za Kikiga na kulinganisha mtindo wa methali za Kiswahili na za Kikiga. Mbinu zilizotumika katika kukusanya data ni hojaji, uchunguzi shirikishi na mahojiano. Nimetumia nadharia ya simiotiki.