ATHARI ZA LUGHA MAMA KATIKA UJIFUNZAJI WA KISWAHILI KAMA LUGHA YA PILI MIONGONI MWA WANAFUNZI WAGANDA WANAOJIFUNZA KISWAHILI
Abstract
Utafiti huu ulishughulikia athari za lugha mama kwa wanafunzi Waganda wanaojifunza lugha yaKiswahili kama lugha ya pili katika wilaya ya Wakiso nchini Uganda.Utafiti huu umegawanyika katika sura tano, sura ya kwanza ni utangulizi, usuli wa mada, suala la
utafiti ambalo ni kuziba athari za lugha mama kwa wanafunzi Waganda wanaojifunza lugha ya Kiswahili, umuhimu wa utafiti ambao ni kusaidia wanafunzi wanaofanya makosa ya kisarufi wakati wa ujifunzaji wa Kiswahili. Mbinu alizotumia mtafiti ni hojaji,
mahojiano,uteuzi wa sampuli ambayo ni matumizi ya vitu vichache kusimamia vitu vingi katika uamuzi wa jumla vifaa vya kukusanya data vikiwemo hojaji yaani kuandikia wahojiwa ili kusaidia wale wasio na muda wa kuulizwa na mahojiano ambayo ni maswali ya kuwauliza wahojiwa macho kwa macho, pamoja na uchanganuzi wa data.Uwasilishaji wa data ambapo ni makosa ya wanafunzi waliyofanya wakati walitunga insha za Kiganda na Kiswahili, matokeo ya utafiti ambayo mtafiti amegundua kwamba lugha ya Kiganda, ina athari kubwa kwa wanafunzi wa Kiswahili ambao ni Waganda wakati wa kutunga insha za Kishwahili.