Kulinganisha ujenzi wa maadili katika riwaya ya Vipuli vya Figo na Ndoto ya Almasi
Abstract
Lengo kuu la utafiti huu lilikuwa kulinganisha ujenzi wa maadili katika riwaya teule za kiswahili
yaani Vipuli vya figo na Ndoto ya Almasi. Malengo mahususi ni a)Kueleza ujenzi wa maadili
katika riwaya ya Vipuli vya figo, Kueleza ujenzi wa maadili katika riwaya ya Ndoto ya Almasi,
Kubainisha tofauti juu ya ujenzi wa maadili katika riwaya za kiswahili yaani Vipuli vya figo na
Ndoto ya Almasi. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya Uhalisia wa kijamaa inayohusisha na
mwanafalsafa Hegel (1971). Msingi wa Uhalisia wa kijamaa unatokana na mawazo ya Karl Marx
ambaye fikra zake zilitokana na mwanafalsafa G.F.Hegel aliyemtangulia Marx na kuathiri falsafa
yake kwa kiasi kikubwa. Utafiti huu ulikuwa utafiti wa maktabani na ulifanyika katika jiji la
Kampala. Kampala iliteuliwa kwa sababu ndipo mahali ambapo maktaba zenye vitabu mbalimbali
zinapatikana ikilinganishwa na sehemu nyingine popote nchini Uganda kwa mfano maktaba ya
Chuo Kikuu cha Makerere na mtafiti alipewa data aliyohitaji kujaza pengo la utafiti. Data za
msingi za utafiti huu zilikusanywa kutoka katika riwaya mbili za Vipuli vya Figo na Emmanuel
Mbogo na Ndoto ya almasi iliyoandikwa na Ken Walibora. Mtafiti alitumia mbinu kadhaa katika
ukusanyaji wa data za utafiti huu ili kukamilisha malengo ya utafiti wake kama vile; mbinu ya
mapitio ya maandishi, mbinu ya hojaji kati ya nyingine. Matokeo ya utafiti pia yanaonesha
kwamba, riwaya hizi mbili zinabainisha tabia za wahusika ambazo zinasawiri maudhui
mbalimbali. Utafiti umegundua kuwa, tabia za wahusika zinaibua maudhui mbalimbali kama vile,
mapenzi, umalaya, umaskini na kadhalika. Zaidi ya hayo, utafiti huu umebaini kuwa waandishi
kwa kiasi kikubwa wanawatumia wahusika kuendeleza maudhui katika riwaya za Kiswahili.
Mwisho kabisa utafiti huu umetoa hitimisho la jumla na mapendekezo kwa watafiti wengine