Kutathmini mchango wa serikali katika ukuzaji na uendelezaji wa lugha ya Kiswahili nchini Uganda
Abstract
Utafiti huu unahusu Kutathimini mchango wa serikali katika ukuzaji na uendelezaji wa lugha ya kiswahili nchini Uganda. Utafiti umegawanyika katika sura tano yaani: sura ya kwanza hadi sura ya tano. Kiswahili ni lugha ya mawasiliano ambayo haijapewa upendo mwingi kwa wanafunzi na wananchi kwa kuzingatia matumizi yake katika nchi kama Uganda. Suala la utafiti huu ni kuchunguza dhima ya serikali katika ukuzaji na uendelezaji wa lugha ya Kiswahili nchini Uganda na kuelemisha wanafunzi wanaosoma Kiswahil kama somo na pia kuelimisha wananchi kuhusu matumizi ya lugha ya Kiswahili nchini Uganda na kwa hivyo serikali ya Uganda inatakiwa kuendelea na shughuli zake za kukuza lugha ya Kiswahili nchini Uganda.
Maswali ya utafiti ambayo ni; Je! Majukumu hayo ya serikali yalitengeneza kitu chochote cha lugha ya Kiswahili nchini Uganda?, Je, serikali ya Uganda imefaulu au haujafaulu katika kukuza lugha ya Kiswahili nchini Uganda?, Ni hatua gani zinazofanywa na serikali ya Uganda kuendeleza lugha ya Kiswahili nchini Uganda?
Sababu za kufanya utafiti huu ni ni kusaidia wananchi kuelewa serikali ya Uganda na jinsi kilivyo kuza Kiswahili katika sehemu mbalimbali za nchi yetu na jinsi Kiswahili kinavyo tumiwa katika shughuli mbalimbali za elimu nchini Uganda, Kupitia utafiti huu, jamii itakuwa na ujuzi juu ya ushairi na fasihi na huko kusaidia watafiti wa mada tofauti kupata maarifa ya jinsi ya kushughulikia utafiti wao. Mtafiti akikumbwa na tatizo la shida la muda ambapo alistahili kukamilisha shughuli zake za utafiti kuhusu suala la utafiti kwa sababu muda haukotosha na kwa hivyo muda ulikuwa mfupi sana kulingana na shughuli zilizohitajika kutekeleza. Mbinu zinazotumiwa na mtafiti ni kama sampuli, vifaa vya kukusanya data vikiwemo Hojaji na mahojiano ili kuchanganua data. Uwasilishaji na uchanganuzi wa data, muhtasari, hitimisho na mapendekezo.