Matumizi ya Nyimbo katika Ufundishaji wa Lugha ya Kiswahili
Abstract
Kuna mbinu nyingi za ufundishaji wa lugha ya kiswahili na mmoja wapo ni mbinu ya nyimbo.Mimi kama mtafiti nilijitolea mhanga na kwenda nyanjani ili kufanya utafiti na kuchunguza vile nyimbo zinavyotumiwa na walimu pamoja na wanafunzi darasani.Katika kazi hii niligundua kwamba nyimbo zinatungwa na walimu wenyewe na kizifundisha kwa wanafunzi darasani.Katika kazi hii nimetia namna nyimbo zinazotumiwa darasani, maoni ya wanafunzi na walimu kuhusu matumizi ya nyimbo na changamoto zinazowakumba na namna ya kuzitatua.