ULINGANISHAJI WA UJAGINA WA WAHUSIKA WANAWAKE KATIKA RIWAYA YA UTENGANO NA ILE YA MSURURU WA USALITI
Abstract
Utafiti huu ulihusu ulinganishaji wa ujagina wa wahusika wanawake baina ya riwaya zaUtengano na Msururu wa Usaliti.Mada hii imefungamana vizuri na lengo la utafiti huulililovunjwa katika malengo mahususi .Malengo hayani kama vile kubaini ukweli na uhalisiaunaozingira swala zima la ujagina wa wahusika wanawake katika riwaya za Utengano na Msururu wa Usaliti na vilevile kubaini changamoto na mafanikio ya kuujenga ujagina wa mwanamke katika jamii ya ubabedume.Ili kutimiza malengo hayo mahususi ya utafiti mtafiti alikusanya data kwa kutumia mbinu ya usomaji makini na upitiaji wa nyaraka mbalimbali
maktabani na kuzichambua kwa kutumia mkabala wa kimaelezo na nadharia ya kifeministi ya
kiafrika.Utafiti huu utawafaa watu wengi kama vile wanafunzi na waadhiri wa chuo kikuu cha Makerere.Vilevile utamsaidia mtafiti kuhitimu shahada yake ya Sanaa ya elimu ,isitoshe itasaidia jamii kwa ujumla katika uundaji wa sera ambazo zitachangia maendeleo ya jinsia ya kike .Mtafiti katika harakati za utafiti wake alikumbwa na changamoto kama vile ukosefu wa hela za
kutosha ,hali mbaya ya anga na mengineyo mengi .Mtafiti alipata kugundua kuwa kulikuwa na vitendo vingi ambavyo vilitendwa na wahusika wanawake na ata uhusika wao ambavyo vilionyesha ujagina katika vipindi tofauti.Hii ni pamoja na nafasi za uongozi ,elimu utetezi,upingaji wa unyanyasaji wa wanaume na uwajibikaji wao kuoinga uovu katika jamii.Mtafiti vilevile alipendekeza uchunguzi zaidi ufanywe katika Nyanja zingine za fasihi ili kudhihirisha ujagina wa wahusika wanawake.Pia alipendekeza vitabu vitabu vitungwe vikiwa na mwelekeo wa kumtukuza mwanamke yaani wakiegemea nadharia ya kifeministi ili ilete usawa
kwa jamii.