Nafasi ya elimu katika ukombozi wa mwanamke : mfano katika riwaya ya Nyuso za Mwanamke
Abstract
Lengo kuu la utafiti huu kulingana na mada ya utafiti lilikuwa kuchunguza nafasi ya elimu katika ukombozi wa mwanamke katika riwaya ya Nyuso za Mwanamke. Vilevile, utafiti huu uliongozwa na malengo makuu mawili ambayo ni; visa vinavyoonesha jinsi mwanamke anavyotumia elimu kujikomboa na changamoto zinazowakumba wanawake wasomi katika harakati za kuleta ukombozi katika riwaya ya Nyuso za Mwanamke. Utafiti huu ulikuwa ni utafiti wa maktabani na ulifanyika katika jiji la Kampala. Kampala iliteuliwa kwa sababu ndipo mahali ambapo maktaba zenye vitabu mbalimbali zinapopatikana ikilinganishwa na sehemu nyingine. Maktaba ya Chuo Kikuu cha Makerere ilitumiwa. Matokeo ya utafiti pia yanaonesha kwamba wanawake wamedharauliwa kwa kupigwa, kutawishwa, kubakwa na kadhalika lakini katika riwaya ya Nyuso za Mwanamke, mhusika msomi Nana alijikomboa na kuleta maendeleo, kipindi cha dukuduku, utajiri, uzalendo ili kupambana na dhuluma zinazomkumba mwanamke. Dhuluma hizi zimewaathiri wanawake kwa njia mbalimbali kama vile ndoa zao kuvunjika. Kwa hivyo, utafiti huu utachochewa kuchunguza na kufafanua juhudi za wanawake wasomi katika kupigania ukombozi na changamoto wanazokutana nazo kurejelea riwaya ya Nyuso za Mwanamke, tunaona nafasi ya elimu katika ukombozi wa mwanamke tukiangalia mhusika msomi Nana. Mwishowe, utafiti huu umetoa hitimisho la jumla na mapendekezo kwa watafiti wengine watakaopenda kuchunguza nafasi ya elimu katika ukombozi wa mwanamke katika kazi za fasihi.