Utamaduni na athari zake katika harakati za ukombozi wa mwanamke. mifano kutoka tamthilia ya Kimya Kimya Kimya na Kilio cha Hhaki
Abstract
Kwanza namshukuru mwenyezi mungu kwa kunipa afya, uwezo na hekima kutekeleza utafiti huu. Shukrani nyingine za dhati kwa chuo Kikuu Cha Makerere hasa idara ya kiswahili na lugha nyingine za kiafrika kwa kunipa msingi timamu katika lugha ya kiswahili ambao umeniongoza hadi siku hii. Tena napitisha shukrani zangu za dhati kwa msimamizi wangu Dkt. Arinaitwe Annensia kwa msaada na ushauri wake katika utekelezaji wa utafiti wangu. Mwenyezi mungu akujalie. Shukrani zisizo na kikomo kwa mamangu mpenzi Bi. Mary Kyokunzire kwa msaada wa kila aina. Asante sana mama kwa Kila jambo ulilonifanyia kuhakikisha kwamba naweza kutimiza ndoto yangu ya kumaliza masomo yangu katika chuo Kikuu. Safari hii haingewezekana bila ushauri wako na msaada wa kifedha. Naomba mwenyezi mungu akubariki na akuongezee miaka ili uweze kujivunia jasho langu. Shukrani nyingine ziwaendee walimu wangu walionifundisha na kunipa msingi thabiti katika lugha ya kiswahili. Wa kwanza ni Mwalimu Bwambale Moses aliyenifundisha kiswahili katika shule ya upili ya St. Mary’s Vocational School, Kyamuhunga. Zisingekuwa nguvu zake, nisingefika kiwango hiki katika lugha ya Kiswahili. Shukrani nyingine ziwaendee walimu wangu katika chuo Kikuu Cha Makerere kama vile Dkt. Innocent Masengo, Dkt. Caesar Jjingo, Dkt. Mutungi Boaz, Bw. Kyomuhendo Victor, Bw. Nelson Nsereko pamoja na Dkt. Asiimwe Caroline. Najivunia kazi mlizonifanyia katika kutimiza ndoto yangu katika lugha ya Kiswahili. Naendelea kuwashukuru ndugu zangu kama vile Kaka Ntare Victor, dada zangu Nakaliika Maxencia na Nakiisekka Anicia, asanteni kwa msaada wenu. Mungu abariki kazi zetu. Mwishoni namshukuru rafiki yangu wa dhati Bi. Kenganzi Lynet kwa yote aliyonifanyia wakati nilipokuwa nakumbana na maisha ya chuo Kikuu. Siwezi kuwataja wote kwa majina. Natambua mchango wa Kila mtu na naomba mungu awabariki.