Changamoto zinazofanya wanafunzi wengi katika ujifunzaji wa Lugha ya Kiswahili
Abstract
Utafiti huu unachunguza changamoto ambazo wanafunzi wanakumbana nayo wakati wa ujifunzaji wa Kiswahili kama lugha ya kigeni katika shule mbalimbali nchini Uganda. Ulibainisha changamoto za wanafunzi ambao wametaka kuzungumza lugha ya Kiswahili lakini mazingira waliyomo, haiwapi fursa ili kuendeleza Kiswahili bali inawahangaisha sana, kwasababu kutokuwa na walimu wa lugha hiyo, ukosefu wa vitabu ,athari za lugha ya Mama na changamoto zingenezo, hivyo basi changamoto za wanafunzi katika kujifunza Kiswahili katika shule za sekondari na kufafanua namna walimu wanavyokabiliana na changamoto katika kufundisha na wanafunzi katika kujifunza Kiswahili hasa haya mazingira ambayo kuna mchanganyiko wa Lugha tofauti.Data za msingi zilikusanywa kwa njia ya hojaji na ushuhudiaji na katika uchambuzi wake ulitumika mkabala wa kimaelezo. Matokeo ya utafiti huu yalibaini kuwa wanafunzi wanakumbana na changamoto ni kutokana na walimu wanapata changamoto katika kufundisha Kiswahili. Miongoni mwao ni walimu kukosa ujuzi wa kutosha wa ufundishaji wa darasa kama hili, ugumu wa kutafsiri wanapokuwa wanafundisha na kulazimika kuchanganya lugha, tafauti za kitamaduni, na nyinginezo. Utafiti ulibaini kuwa wanafunzi wanapata changamoto za tafauti za kiutamaduni, hadhi zao, athari ya lugha ya kwanza katika kujifunza lugha ya Kiswahili. Utafiti ulipendekeza kuwa; walimu wapatiwe mafunzo ya kutosha katika kufundisha Kiswahili kwa wanafunzi wanaojifunza Kiswahili, walimu wajifunze lugha nyengine za kigeni pamoja na utamaduni wake. Vilevile wawe na ubunifu wa kutumia mbinu na viwezeshi muafaka pamoja na zana za kisasa kwa madarasa kama haya. Kwa upande wa wanafunzi kuzungumza lugha ya Kiswahili darasani, kuheshimu utamaduni wa kila mwanafunzi, kutotilia maanani tafauti ya mwanafunzi mmoja na mwengine na nyenginezo.