Taswira ya mwanamke katika Nyimbo za Kisasa za ‘Bongo Fleva
Abstract
Utafiti huu unachunguza Taswira ya mwanamke katika nyimbo za kisasa Bongo Fleva: mfano kutoka nyimbo teule za Jose Chameleon kutoka nchini Uganda na nyimbo zake kama Jamila na Bei kali, Darassa kutoka nchini Kenya na nyimbo zake kama give up na Nikiondoka, Diamond Platinum kutoka nchini Tanzania na nyimbo zake kama Yatapita na kamwambie. Mada hii imefungamana vizuri na lengo kuu la utafiti huu ambayo ni kuchunguza jinsi mwanamke anavyosawiriwa na wasanii wa kisasa. lilivunjwa katika malengo mahususi tatu. Malengo hayo ni: (i) Kuelewa maisha na historia ya wasanii kama Diamond Platinumz, “Dkt”. Jose Chameleon na Darassa. (ii) Kubainisha maudhui ya taswira ya mwanamke katika nyimbo za Diamond Platinumz, “Dkt”. Jose Chameleon na Darassa kutoka nchi mbili za Afrika Mashariki na la mwisho ni Kuchunguza iwapo nyimbo hizo zinajikita kwenye masuala ya kijinsia kwa njia ya kuhamasisha usawa wa kijinsia au kuchochea ubaguzi wa kijinsia kwa kumchora mwanamke pekee katika nyimbo hizo. Ili kutimiza malengo ya utafiti huu, data zilikusanywa kwa kutumia mbinu za, upekuzi wa yaliyomo, upitiaji wa nyaraka na mahojiano ili kukusanya data. Data za utafiti huu zilishughulikiwa kupitia mbinu ya msingi na mbinu ya upili. Data za msingi zilikusanywa kupitia upekuzi wa yaliyomo na mahojiano, ilhali data za upili zilikusanywa Kwa kutumia upitiaji wa nyaraka zilizokwishafanyiwa utafiti mtandaoni. Nadharia ya Uchanganuzi Nafsia katika mtazamo wa kike ndio iliongoza utafiti huu kwa kutoa fasili zaidi kuhusu taswira ya mwanamke. Matokeo ya utafiti huu yalibaini kuwa mwanamke ni mpenda starehe hata bila kutumia mali au pesa zake mwenyewe bali za mwanaume, mwanamke ni kiumbe wa kuachwa na mume wake, mwanamke ni kiumbe muovu, mwanamke ni kiumbe tegemezi, mwanamke ni kiumbe wa kujifunza kwa tajriba na mwisho kuwa ni mtu wa nipe nikupe (malaya)