dc.contributor.author | Aminga, Deborah | |
dc.date | 2018 | |
dc.date.accessioned | 2018-10-22T12:56:47Z | |
dc.date.available | 2018-10-22T12:56:47Z | |
dc.identifier.uri | http://hdl.handle.net/20.500.12281/4799 | |
dc.description.abstract | Tasnifu hii imeonyesha usawiri wa wahusika vijana wavulana na wasichana katika riwaya za Kufa Kuzikana, Kidagaa kimemwozea na Nyota ya Rehema. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya uyakinifu wa kijamii ambao unajihusisha na utetezi wa wanyonge na ukombozi wao. Tumetambua kwamba vijana ni mawakala wa mabadiliko na wanaweza kuleta mchango ambao unaweza kuwafaidi wanajamii wote. Hii ni kwa sababu vijana ni wenye nguvu za mwili na maarifa ambayo wanaweza kutumia ili kuifunza jamii. Pamoja na haya, imeonyesha kwamba vijana wanakabiliana na changamoto nyingi ambazo ni lazima zichukuliwe hatua ili kizazi hiki ambacho ni muhimu sana kipate kuokolewa. Mbinu za utafiti zilizotumiwa ni za kimaktaba na utathmini wa matini. Maktabani, riwaya za kufa kuzikana, kidagaa kimemwozea na Nyota ya Rehema, makala tofauti kama vile tasnifu na vitabu vyenye maelezo kuhusu nadharia ya uyakinifu wa kijamii ilisomwa. Kwenye mtandao masuala yanayohusiana na vijana yalisomwa na kuangaliwa na pia kusoma maelezo kuhusu nadharia ya uyakinifu wa kijamii. | |
dc.subject | Literature | |
dc.subject | Youth characterisation | |
dc.title | Usawiri wa wahusika vijana(wavulana na wasichana) katika riwaya za kufa kuzikana, kidagaa kimemwozea na nyota ya rehema | en_US |
dc.title.alternative | Characterisation of the youth in Novels of Kufa kuzikana, Kidagaa kimemwozea and Nyota ya rehema | |