Sanaa ya mtego inavyowasilishwa katika tamthilia ya Mtego na jinsi inatumika kuendeleza maudhui na Sanaa zingine
Sanaa ya mtego inavyowasilishwa katika tamthilia ya Mtego na jinsi inatumika kuendeleza maudhui na Sanaa zingine
Date
2023
Authors
Achuka, Lobee Boniface
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Makerere University
Abstract
Lengo kuu la huu lilikuwa ni kuchunguza namna sanaa ya mtego inavyowasilishwa katika tamthilia ya Mtego na jinsi sanaa hiyo inatumika kuendeleza maudhui na sanaa zingine katika tungo hilo. Pia, malengo mahususi yalikuwa matatu; kubaini sanaa ya mtego katika tamthilia ya Mtego, jinsi sanaa hiyo ya mtego imetumika kuendeleza maudhui na kutambua sanaa zingine ambazo zinajitokeza katika tamthilia lengwa. Utafiti huu ulikuwa ni utafiti wa maktabani na ulifanyika katika maktaba kuu ya Chuo Kikuu cha Makerere aabayo iliteiliwa kwa kuwepo karibu na mtafiti na kuwa na vifaa muhimu vya kurahisisha na kufanikisha utafiti huu kama vile magazeti, majarida tafiti za kale, kompyuta na mtandao bora. Matokeo ya utafiti yanaonesha kwamba sanaa ya mtego inajitokeza kwa shughuli kama vile ndoa za jinsia moja, kandanda, demokrasia, usawa wa kijinsia, elimu ya kisasa, pesa, mavazi ya kisasa na UKIMWI. Vilevile, mitego hiyo zimetumika kuendeleza maudhui kama vile ukoloni mamboleo, nafasi ya mwanamke katika jamii, migogoro, usaliti, maovu, sheria na kadhalija. Pia sanaa zingine kama vile muundo, umbo, mandhari na mpangilio wa vitendo na maonesho zilijitokeza katika tamthilia ya Mtego. Mwisho, utafiti huu umetoa hitimisho wa jumla na kutoa mapendekezo kwa watafiti wengine watakaopenda kuchunguza sanaa mbalimbali na uendelezaji maudhui.
Description
Tasnifu ya utafiti inayowasilishwa katika Taasisi ya Lugha na Mawasiliano Kitivo Cha Lugha za Kiafrika ili kutekeleza baadhi ya mahitaji ya Shahada ya Kwanza ya sanaa ya Ualimu ya Chuo Kikuu cha Makerere
Keywords
Citation
Achuka, L. B. (2023). Sanaa ya mtego inavyowasilishwa katika tamthilia ya Mtego na jinsi inatumika kuendeleza maudhui na Sanaa zingine (Unpublished undergraduate dissertation). Makerere University, Kampala, Uganda.