Udadis wa namna bora ya kutumia mtindo katika utunzi wa fasihi andishi : mfano wa Riwaya ya Utengano

Date
2024
Authors
Kavuma, Muhammad Abasi
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Makerere University
Abstract
Tasnifu hii inahusu kazi ya utafiti iliyoandikwa juu ya mada ya UDADIS WA NAMNA BORA YA KUTUMIA MTINDO KATIKA UTUNZI WA FASIHI ANDISHI: MFANO WA RIWAYA YA UTENGANO. Tasnifu hii ni mojawapo ya vigezo mbalimbali ambavyo wanafunzi sharti watimize kabla ya kupata shada yao ya kwanza. Kazi imechunguza suala zima la matumizi bora ya mtindo kipengele mojwapo cha fani ya kazi ya fasihi andishi. Mtindo umezingatiwa katika kazi hii kwa sababu nyingi kati ya kazi za fasihi andishii hukosa hadhira na hivyo kufa mapema kwa sababu ya makossa ya kimtindo. Lengo kuu la kazi hii ni kubaini namna ambavyo wandishi wa kazi za fasihi andishi hutumia kipengele cha mtindo kuwasilisha kazi zao. Lengo hili limeendewa kupitia hatua mahususi tatu yaani, kwanza kabisa ni kutoa mifano ya aina za mitindo inayotumiwa katika uwasilishaji wa fasihi andishi, pili tulionesha namna bora ya kutumia mitindo hii katika kutunga kazi za kifasihi na mwisho kabisa kazi ulijadili baadhi ya makossa ambayo hutendwa na watunzi wa fasihi andishi wanapotumia mitindo mbalimbal. Utafiti huu umetumia mbinu ya upekuzi wa yaliyomo. Yaani, tunaweza kusema upekuzi uliofanywa hapa ni ule wa kimaktaba ambapo marejeo mbalimbali yamepitiwa hasa riwaya ya Utengano (1980). Utafiti umegundua kwamba makossa mengi yanayofanyika katika matumizi ya mtindo hupatikana katika kazi nnyingi za wandishi chipuzi. Jambo hili tumelibaini kupitia kutizama kazi yake ya Utengano (1980) ambayo ni miongoni mwa kazi alizozitoa mwanzoni na kuiliganisha na zile za hivi karibuni kama vile Dunia Yao (2006), tunaona kwamba pamoja na kuwa mwandishi huyu anadhihirisha ustadi mkubwa wa umilisi wa lugha, ipo tofauti kubwa kati ya uchaguzi wa msamiati kati ya riwaya hizi mbili ambapo kuna umakini mwingi uliotumika katika ile ya Dunia Yao (2006) ukilinganisha na ile ya Utengano (1980). Kwa muhtasari tunaweza kusema kwamba mtindo ni kipengele amabacho hutambulisha kiwango cha ufundi wa mtunzi kwa hadhira na ipo haja kubwa ya watu kuelimishwa juu ya namna bora ya kukitumia ili kuepukana na makosa ya kizembe yanayorudisha nyuma maedeleo ya fasihi. Hivyo basi, utafiti huu unapendekeza kwamba ipo haja kubwa ya kutizama upya matumizi ya vipengele vingine vya kazi ya fasi hasa vile vya fani kwa sababu bila ya umbo la nje kuboreshwa, la ndani pia haliwezi kuboreshwa.
Description
Tasinifu iliyowasilishwa kwa ajili ya kukamilisha baadhi ya masharti ya Digrii ya kwanza (BARS) (Kiswahili) ya chuo kikuu cha Makerere
Keywords
Style in Literature, Kiswahili written literature, Style in written literature
Citation
Kavuma, M. A. (2024). Udadis wa namna bora ya kutumia mtindo katika utunzi wa fasihi andishi : mfano wa Riwaya ya Utengano (Unpublished undergraduate dissertation). Makerere University, Kampala, Uganda