Mchango wa tehama katika ufundishaji wa insha za Kiswahili katika shule za upili Wilayani Wakiso nchini Uganda
Mchango wa tehama katika ufundishaji wa insha za Kiswahili katika shule za upili Wilayani Wakiso nchini Uganda
| dc.contributor.author | Nteyera, Kisembo Shillah | |
| dc.date.accessioned | 2024-12-05T15:45:41Z | |
| dc.date.available | 2024-12-05T15:45:41Z | |
| dc.date.issued | 2024-08 | |
| dc.description | Tasnifu iliyowasilishwa katika Idara ya Lugha za Kiafrika kwa Madhumuni ya kutosheleza baadhi ya mahitaji ya Shahada ya Kwanza ya Ualimu, Chuo Kikuu Cha Makerere | en_US |
| dc.description.abstract | Teknnolojia ya Habari na mawasiliano (TEHAMA) imeleta mapinduzi makubwa katika sekta ya elimu, ikiwemo ufundishaji wa insha za Kiswahili katika shule za upili. Kwa kutumia TEHAMA waalimu na wanafunzi wataweza kuboresha mbinu na ufanisi wa kujifunza lugha ya kiswahili hasa katika uandishi wa insha, ambao ni sehemu muhimu ya mtaala. Kwanza, TEHAMA imewezasha upatikanaji wa rasilimali na vifaa vya kujifunzia kupitia mtandao. Walimu wanaweza kufikia maktaba za kidijitali, majarida na blogu za lugha ambazo zinztoa mifano ya insha bora. Hii inawasaidia wanafunzi kupata mifano mbalimbali ya uandishi na hivyo kuboresha uwezo wao wa kuandika insha za Kiswahili kwa ufasaha. Kwa mujibu wa Msuya (2020), matumizi ya maktaba za kidijitali yameongeza ufahamu na maarifa miongoni mwa wanafunzi wa lugha. Pili, zana za TEHAMA kama vile programu za kuhariri maandishi na mifumo ya kujifunza kwa njia ya mtandao (LMS) zimeimarisha mawasiliano na ushirikiano kati ya walimu na wanafunzi. Walimu wanaweza kutoa maoni na marekebiso ya insha kwa haraka kupitia barua pepe au majukwaa ya kidijitali, kama vile “google classroom” Hii inawawezesha wanafunzi kupata mrejesho wa haraka na kurekebisha makosa yao, hivyo kujifunza kwa njia endelevu (Ndung’u, 2019) Aidha, TEHAMA Imewezesha ujifunzaji wa kujitegemea na wa kibinafsi ambapo wanafunzi wanaweza kutumia programu za kujifunza lugha kama “duolingo”, ambazo zinzwawezesha kufanya mazoezi ya sarufi na msamiati kwa njia ya kuvutia na ya mwingiliano. Hii inawasaidia wanafunzi kuimarisha ujuzi wao wa lugha bila kutegemea sana mwalimu. Mwishowe, mchango wa TEHAMA katika ufundishaji wa insha za Kiswahili katika shule za upili ni mkubwa na wa manufaa. Imeweza kuboresha upatikanaji wa rasilimali, kuimarisha mawasiliano na kutoa fursa za kujifunza kibinafsi, hii inasaidia wanafunzi kuwa na uelewa mzuri wa lugha ya Kiswahili na hivyo kuwa na uwezo mkubwa wa kuandika na vile kubuni insha bora za kiswahili. | en_US |
| dc.identifier.citation | Nteyera, K. S. (2024). Mchango wa tehama katika ufundishaji wa insha za Kiswahili katika shule za upili Wilayani Wakiso nchini Uganda; unpublished dissertation, Makerere University, Kampala | en_US |
| dc.identifier.uri | http://hdl.handle.net/20.500.12281/19884 | |
| dc.language.iso | en | en_US |
| dc.publisher | Makerere University | en_US |
| dc.subject | Tehama katika ufundishaji wa insha za Kiswahili | en_US |
| dc.title | Mchango wa tehama katika ufundishaji wa insha za Kiswahili katika shule za upili Wilayani Wakiso nchini Uganda | en_US |
| dc.type | Thesis | en_US |