Uchambuzi wa tamthilia ya Mkwamo na Kilio Cha Haki kwa kutumia nadharia ya Umaksi
Abstract
Lengo kuu la utafiti huu lilikuwa uchambuzi wa Tamthilia ya Mkwamo na Kilio cha Haki kwa kutumia Nadharia ya Umaksi. Malengo mahususi ya utafiti huu yalikuwa ni; udhihirishaji wa matumizi ya nadharia ya Umaksi katika tamthilia ya Mkwamo, pia na udhihirishaji wa matumizi ya nadharia ya umaksi katika tamthilia ya Kilio cha Haki. Utafiti huu ulikuwa ni utafiti wa maktabani na ulifanyika katika jiji la Kampala.Kampala iliteuliwa kwasababu ndipo mahali ambapo maktaba zenye vitabu mbalimbali zinapatikana ikilinganishwa na sehemu nyingine.Nilitumia maktaba ya Chuo Kikuu cha Makerere.Matokeo ya utafiti yanaonesha kwamba tamthilia hizi mbili zinaonesha matumizi ya nadharia ya umaksi.Utafiti umegundua kuwa tamthilia ya Mkwamo na Kilio cha Haki zinatumia nadharia ya umaksi kama vile uongozi mbaya wa kunyanyasa na kukandamiza wenyeji wa Kasulenge inayoongozwa na mfalme Mkazo,dola,harakati za utabaka(tabaka la chini na tabaka la juu),umaskini na biashara (katika tamthilia ya Kilio cha Haki). Katika utafiti huu, mbinu zilizotumiwa kukusanya data ni usomaji kwa makini. Kwa hivyo ninapendekeza kuwa watafiti wengine wazifanyie utafiti zaidi tamthilia hizi mbili kwa kutumia nadharia nyingine kama umuundo, uhalsia. Kubaini matumizi ya lugha na dhamira kuu za vitabu hivi. Mwisho kabisa utafiti huu umetoa hitimisho na kwa ujumla mapendekezo kwa watafiti wengine watakaopenda kuchunguza matumizi ya nadharia ya umaksi.