Nafasi ya mwanamke katika ukombozi wa jamii: mfano wa tamthilia; Kimya kimya kimya na Chema chajiuza
Abstract
Lengo kuu la utafiti huu kulingana na mada ya utafiti lilikuwa kuchunguza nafasi ya mwanamke katika ukombozi wa jamii kwa kupata mifano kutoka tamthilia za Kimya Kimya Kimya na Chema Chajiuza. Vilevile, utafiti huu uliongozwa na malengo makuu mawili ambayo ni; Kubaini nafasi hasi ya mwanamke katika Tamthilia ya Kimya Kimya Kimya na Chema Chajiuza na Kufafanua jinsi mwanamke anavyopambana na changamoto zinazotishia maisha yake katika Tamthilia ya Kimya Kimya Kimya na Chema Chajiuza ukiongozwa na nadharia ya ufeministi.Utafiti huu ulikuwa utafiti wa maktabani na ulifanyika kijijini Kampala katika maktaba ya Chuo Kikuu cha Makerere kwasababu ndio pahali yenye vitabu vilivyotakiwa yaani Chema Chajiuza na Kimya Kimya pamoja na marejeleo maalum. Matokeo ya utafiti huu yanaonyesha namna ambazo mwanamke anachorwa na nafasi hasi kama, kuwa mnyonge, kudharauliwa na mwanamme, kuachwa nyumbani na kadhalika. Vilevile, uwezo wa mwanamke unaonyeshwa yaani vile mwanamke anaweza kufanya ili kukomboa jamii yake kama; kuwa jasiri, mwenye heshima, mzalendo, msema ukweli na kadhalika ukiongozwa na tamthilia mbili teule Kimya Kimya Kimya na Chema Chajiuza. Utafiti huu unapendekeza kuwa watafiti wa kazi za fasihi wanaotafiti kuhusu taswira ya mhusika mwanamke wazingatie muktadha wa ukombozi na maendeleo ya jamii husika tangu taswira hii inaweza kubadilika kutegemea muktadha wa jamii na muda na tangu fasihi kama kioo cha jamii huakisi matukio katika jamii.