Elimu kama chombo cha ukombozi wa mwanamke katika riwaya ya Nguvu ya Sala

Date
2023-01
Authors
Kasaija, Bonefance
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Makerere University
Abstract
Utafiti huu unahusu elimu kama chombo cha ukombozi wa mwanamke katika riwaya Nguvu ya Sala. Usawiri wa mwanamke ambaye ni msomi katika jamii na yule ambaye hajasoma na anavyonyimwa kwa baadhi ya haki. Malengo ya utafiti huu ni Kuchunguza nafasi ya mwanamke msomi anavyopigania haki katika riwaya Nguvu ya Sala na la pili ni Kubainisha mchango wa mwanamke msomi katika ujenzi wa jamii katika riwaya Nguvu ya Sala. Utafiti huu unatathimini ni kiwango gani mwanamke anavyochangia kupigania haki zake baada ya kupata elimu. Ili kufikia malengo ya utafiti huu, Wanawake wanapaswa kufanya kazi pamoja, kama shirika moja linalopigania jingine kama inavyoonyeshwa katika riwaya Nguvu ya Sala.
Description
Tasnifu iliyowasilishwa kwa idara ya Lugha za Kiafrika ili kutimiza baadhi ya mahitaji ya kutunikiwa Shahada ya Sanaa na Ualimu ya Chuo Kikuu Cha Makerere
Keywords
Ukombozi wa mwanamke
Citation
Kasaija, B. (2023). Elimu kama chombo cha ukombozi wa mwanamke katika riwaya ya Nguvu ya Sala; unpublished dissertation, Makerere University, Kampala