Ufaafu wa Istilahi za Kiswahili katika Vitabu Rasmi vya NCDC kwa Mtaala Mpya wa Umilisi nchini Uganda
Ufaafu wa Istilahi za Kiswahili katika Vitabu Rasmi vya NCDC kwa Mtaala Mpya wa Umilisi nchini Uganda
Date
2025-10-13
Authors
Nizeyimana, Richard
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Makerere University
Abstract
Utafiti huu unachunguza ufaafu wa istilahi za Kiswahili zinazotumika katika vitabu vya mtaala mpya wa umilisi wa shule za sekondari nchini Uganda ukizingatia vigezo vya PEGITOSCA na kanuni nyingine za usanifishaji wa istilahi za Kiswahili. Utafiti ulipima istilahi 50 kutoka vitabu rasmi vya NCDC (2020) ili kubaini ubora wake katika matumizi ya kielimu. Matokeo yalionyesha kuwa 70% ya istilahi ni faafu, ingawa changamoto kuu zilibainika katika umataifa, uangavu, na uchumi wa lugha. Mahojiano na walimu yalionyesha kuwa istilahi nyingi ni ndefu, ngumu kueleweka, na hazilingani na lugha ya mawasiliano darasani. Utafiti unahitimisha kuwa mfumo wa istilahi za Kiswahili katika mtaala wa NCDC una msingi thabiti wa kilugha, lakini unahitaji maboresho ya kimkakati ili kuongeza uwazi, urahisi wa matumizi, na mashiko ya kimataifa katika elimu ya sekondari.
Description
Tasnifu iliyowasilishwa kwa idara ya lugha za kiafrika ili kutimiza baadhi ya mahitaji ya kuhitimu shahada ya ualimu ya chuo kikuu cha Makerere
Keywords
Istilahi za Kiswahili, Kiswahili Terminology, Terminology development, PEGITOSCA, NCDC books, Competency Based Curriculum, language policy, elimu ya kiswahili
Citation
Nizeyimana, R. (2025). Ufaafu wa Istilahi za Kiswahili katika Vitabu Rasmi vya NCDC kwa Mtaala Mpya wa Umilisi nchini Uganda (Unpublished undergraduate dissertation) Makerere University, Kampala, Uganda