Kulinganisha taswira ya mapenzi katika nyimbo za Kiswahili za Kimapokeo na za Kisasa

Date
2026
Authors
Muchika, Abdukarimu.
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Makerere University
Abstract
Utafiti huu ulichunguza na kulinganisha taswira ya mapenzi katika nyimbo za Kiswahili za kimapokeo na za kisasa. Lengo kuu lilikuwa kubaini mfanano na tofauti katika namna taswira za mapenzi zinavyowasilishwa katika aina hizi mbili za nyimbo. Utafiti uliongozwa na Nadharia ya Uhakiki wa Kimuundo na ulitumia mbinu ya uchanganuzi wa nyaraka. Data ilipatikana kutoka katika nyimbo kumi, ambapo tano zilikuwa za kimapokeo na tano za kisasa, zilizochaguliwa kwa kutumia usampulishaji lengwa. Uchambuzi wa data ulifanywa kwa kutumia uchanganuzi wa kimaudhui kwa kuzingatia maneno, ishara na taswira zilizojitokeza katika nyimbo hizo. Matokeo ya utafiti yalionyesha kuwa nyimbo za kimapokeo zilitumia taswira za upendo, uaminifu, uzuri, utamu, maumivu, huzuni, migogoro na matumaini. Taswira hizo zilijengwa kwa kutumia vitu kama ua, tufaha na ndege. Kwa upande wa nyimbo za kisasa, taswira hizo pia zilijitokeza, lakini ziliambatana na mazingira ya sasa kama moyo, fedha, kazi, chakula, safari na maisha ya mjini. Utafiti pia ulibaini kuwa kuna mfanano katika hisia za msingi za mapenzi, lakini tofauti zimeonekana katika vitu, lugha na mazingira yanayotumiwa kuziwasilisha. Aidha, mabadiliko ya kijamii, kiuchumi na kiteknolojia yameathiri namna taswira za mapenzi zinavyowasilishwa katika nyimbo za kisasa. Kwa ujumla, utafiti umehitimisha kuwa hisia za msingi za mapenzi zimeendelea kuwepo katika nyimbo za kimapokeo na za kisasa, ingawa namna ya kuzitambulisha na kuziwasilisha imebadilika kulingana na mazingira ya jamii.
Description
Tasnifu ya utafiti inayowasilishwa katika idara ya Lugha za Kiafrika Kwa Ajili ya Kutosheleza Baadhi ya Masharti ya Kuhitimu Shahada ya Ualimu ya Chuo Kikuu cha Makerere
Keywords
Citation
Muchika, A. (2026). Kulinganisha taswira ya mapenzi katika nyimbo za Kiswahili za Kimapokeo na za Kisasa; Unpublished dissertation, Makerere University, Kampala.