Kulinganisha Maudhui ya ukoloni katika tamthilia ya Mzalendo Kimathi na Kilio Cha Haki

Date
2022-10-25
Authors
Mucunguzi, Joan
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Makerere University
Abstract
Tamthilia ni utanzu wa fasihi ambao huwasilisha ujumbe wake kwa njia ya usimulizi ama kimaandishi. Kwa mujibu wa Wamitila (2007), huu ni utanzu ambao huandikwa kwa mtindo wa mazugumzo ya wahusika. Tamthlia ambazo tuliteua zilibeba maudhui ya ukoloni ndani yaani Mzalendo Kimathi na Kilio Cha Haki. Aidha, Wamitila anasema kwamba maudhui ni jumla ya mambo yote yanayozungmziwa katika kazi ya kifasihi. Katika utafiti huu tutachunguza maudhui ya utawala ya kikoloni kwa kulinganisha tamthiliya ya Mzalendo Kimathi na ya Kilio cha Haki ili kugundua usawili wa ukoloni katika kazi hizi za Fasihi. Fasihi ni sanaa inayotumia lugha bunifu ili kueleza tajriba mbalimbali za maisha ya wanajamii. Njogu na Chimerah (1999) wanaeleza kuwa fasihi inawasilisha hali, mwingiliano, mivutano na mikinzano miongoni mwa binadamu na mazingira yake. Utafiti huu unahusu ulinganishaji wa maudhui ya utawala ya Kikoloni katika tamthilia mbili za Kiswahili. Hapa tunachunguza jinsi waandishi wa tamthilia walivyosawiri maudhui ya ukoloni katika kazi zao za fasihi.
Description
Tasinifu ya utafiti iliyowasilishwa katika idara ya lugha za kiAfrika kutimiza baadhi ya mahitaji ya shahada ya Kwanza ya chuo kikuu Cha Makerere
Keywords
Ukoloni, Mzalendo Kimathi, Kilio Cha Haki
Citation
Mucunguzi, J. (2022). Kulinganisha Maudhui ya ukoloni katika tamthilia ya Mzalendo Kimathi na Kilio Cha Haki (Unpublished undergraduate dissertation). Makerere University, Kampala Uganda