Show simple item record

dc.contributor.authorKABUGHO, FELESTUS
dc.date.accessioned2021-04-06T09:23:30Z
dc.date.available2021-04-06T09:23:30Z
dc.date.issued2021-04-06
dc.identifier.urihttp://hdl.handle.net/20.500.12281/10003
dc.descriptionen_US
dc.description.abstractUtafiti huu ulihusu uchunguzi linganishi wa nafasi ya mwanamke katika utenzi wa Mwana Kupona na ule katika utamaduni wa Kikonzo. Mwana Kupona ni utungo unaomsawiri mwanamke kuonyesha tabia nzuri kwa mumewe bila tofauti, Mwanamke katika utamaduni wa kikonzo anasawiriwa kama mkakamavu na mwenye heshima kwa mumewe kiutendaji kama vile kumkaribisha vizuri mwanamume na kumpigia magoti. Suala la utafiti lilikuwa ni kuchunguza kuchunguza uhusiano uliopo kati ya nafasi ya mwanamke katika utenzi wa Mwana Kupona na ule katika utamaduni wa Kikonzo ili kuinua tabia za wanawake katika familia zao. Lengo kuu la utafiti huu lilikuwa ni kuchunguza uhusiano uliopo katika nafasi ya mwanamke katika utenzi wa Mwana Kupona na katika utamaduni wa jamii ya Kikonzo. Malengo mahususi yalikuwa Kulinganisha hadhi ya mwanamke katika utenzi wa Mwana Kupona na utamaduni wa Kikonzo, kuchunguza majukumu ya mwanamke katika utenzi wa Mwana Kupona na utamaduni wa Kikonzo na kutambua changamoto zinazomkumba mwanamke wa Kikonzo na yule wa utenzi wa Mwana Kupona. Maswali ya utafiti yalikuwa; ni hadhi ipi inayopewa mwanamke katika utenzi wa Mwana Kupona na yule mwanamke katika utamaduni wa Kikonzo?, ni majukumu yapi yanayopewa mwanamke katika utenzi wa Mwana Kupona na yule katika utamaduni wa Kikonzo? na ni changamoto zipi zinazomkumba mwanamke katika utenzi wa Mwana Kupona na yule katika utamaduni wa Kikonzo? Utafiti huu uliwezesha mtafiti kutimiza baadhi ya mahitaji ya kuhitimu shahada ya sanaa na elimu ya Chuo Kikuu cha Makerere. Pia ulimsaidia mtafiti na waliohusika kuchunguza majukumu ya mwanamke katika utenzi wa Mwana Kupona na ule wa utamaduni wa Kikonzo na tamaduni mningine. Matokeo ya utafiti huu watawawezesha watafiti wajao kupata marejeleo na utafiti huu utakuwa kama kukumbukumbu katika kitivo cha elimu katika chuo kikuu cha Makerere. Utafiti ulifanyiwa katika eneo la Bwera wilayani Kasese nchini Uganda na katika vijiji vya Karambi na Bwera ambapo mtafiti atawahoji watu thelathini (30) ambao wako katikati ya miaka 23-55. Kwa sababu hao wana uzoefu kuhusu maisha ya familia. Kwa hivyo walikisiwa huwa na ujumbe uliotosha kuhusu mada hii. Pia, mtafiti alitumia utenzi wa Mwana Kupona na kazi zingine zenye ujumbe kuhusu mada hii. Kuhusu wakati, mtafiti alitumia muda wa miezi miwili kuanzia Oktoba hadi Desemba ili kupata ujumbe uliokamilika. Mtafiti pia alitumia mbinu za kukusanya data kama hojaji, mahojiano na uchunguzi shirikishi kukusanya data.en_US
dc.subjectMwanamke
dc.subjectKikonzo
dc.titleUchunguzi linganishi wa nafasi ya mwanamke katika utenzi wa mwana kupona na utamaduni wa kikonzoen_US


Files in this item

Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record