Athari za mazingira ya mwandishikatika Udhihishhaji wa Maudhui katika riwaya teule za Kiswahili
Abstract
Ningependa kuchukua fursa hii kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuniwezesha kufikia hatua hii ya kukamilisha utafiti huu nilioufanya kwa miezi kadhaa. Yeye ndiye aliyenijalia nguvu, uwezo wa fikra na utashi wa kufanya utafiti huu ambao leo hii nauhitimisha. Kwake yeye Mungu nasema AsanteMungu kwa yote ulionitendea.
Napenda pia kutumia fursa hii kumshukuru sana msimamizi wangu Bw. Nelson Nsereko kwa kunifundisha na kuniongoza katika utafiti huu mpaka hatua hii tuliyofikia hivi sasa. Mhadhiri wangu hakuchoka katika kunielekeza na kunitia moyo hata pale nilipoonekana kukata tamaa. Mhadhiri wangu alinitaka niwe mvumilivu kwani siku moja nitamaliza shule na kutunukiwa shahada yangu.
Napenda pia kuishukuru familia yangu kwa kunijali na kunipenda. Watu wa familia yangu wamekuwa bega kwa bega na mimi katika kipindi chote cha masomo yangu kuanzia mwanzo mpaka mwisho. Kwa hakika sina cha kuwalipa zaidi ya kuwaombea dua kwa Mwenyezi Mungu Wingi wa rehema na mwenye kurehemu. Mwenyezi Mungu awalipe malipo mema.