Show simple item record

dc.contributor.authorTumutangirire, Acleo
dc.date.accessioned2023-02-21T09:48:21Z
dc.date.available2023-02-21T09:48:21Z
dc.date.issued2023-02-10
dc.identifier.citationTumutangirire, A. (2023). UCHANGANUZI WA TAMTHILIA YA MFALME EDIPODE KAMA KAZI YA UHALISIAJABU. ( Unpublished Undergraduate Dissertation). Makerere University, Kampala, Uganda.en_US
dc.identifier.urihttp://hdl.handle.net/20.500.12281/15723
dc.descriptionA MATINI ILIYOWASILISHWA KWA AJILI YA KUTOSHELEZA BAADHI YA MAHITAJI YA SHAHADA YA SANAA YA UALIMU (BAED) KATIKA CHUO KIKUU CHA MAKERERE. A dissertation submitted to the College of Education and External Studies in partial fulfillment of the requirements of the award of the degree of Bachelor of Arts with Education of Makerere University.en_US
dc.description.abstractMatini hii inahusu uhalisiajabu katika tamthilia ya Mfalme Edipode ya Sofokile. Katika matini hii nimechunguza uhalisiajabu katika kiwango cha wahusika na mandhari katika tamthilia hii nikiongozwa na nadharia ya Uhalisiajabu. Ili kufikia lengo langu, matini hii imegawanywa katika sehemu mbalimbali yaani; Utangulizi, mwili na hitimisho. Katika mwili wa matini hii, vipengele vya Uhalisiajabu vimechunguzwa na kubainishwa katika viwango vya wahusika na mandhari yenye matukio ya Uhalisiajabu. Vile vile,Matini hii imechanganua tamthilia ya Mfalme Edipode kwa kuegemea nadharia ya uhalisiajabu. Uhalisiajabu umeathiri kazi za kifasihi kwa upana na hujitokeza kwa namna mbalimbali. Suala la uhalisiajabu linafaa kuchunguzwa kwa sababu maisha yetu ya leo na hata jamii tunamoishi yametawaliwa na matendo ya kiajabu ambayo kwa kawaida hutuhangaisha na kutukanganya. Ukilinganisha na aina nyingine za nadharia zinazoyaendeleza na kuyaathiri maisha yetu, uhalisiajabu unajitokeza kwa kiasi kikubwa ingawa huwa vigumu kwa baadhi ya binadamu kutambua kwa urahisi kuwa madhara yake huenda yakawa hatari zaidi. Aidha, kama kazi nyingine za fasihi zile, matendo yanayotendeka katika tamthilia ya Mfalme Edipode yanalenga kufunza na kuboresha jamii zetu hasa tukirejelea hatendo hayo kwa jicho la uangalifu. Vile vile, lugha iliyotumiwa katika tamthilia nzima inalingana sana na ya mazungumzo yetu ya kawaida kwa sababu zote hurejelea mitagusano ya kijamii ambapo wahusika hujibizana/huzungumzana moja kwa moja kuhusu mambo tofauti tofauti. Kwa kutumia nadharia ya uhalisiajabu kwa hiyo,matini hii, inadhihirisha kwamba baadhi ya mambo binadamu anayoyapitia huwa ya kutishia, ya kiajabu na ya kifantasia zaidi na huenda yakaathiri mkondo wa maisha yake.en_US
dc.description.sponsorshipprivateen_US
dc.language.isootheren_US
dc.publisherMakerere Universityen_US
dc.subjectPlaysen_US
dc.subjectRealismen_US
dc.subjectKing Oedipusen_US
dc.subjectOral literatureen_US
dc.titleUCHANGANUZI WA TAMTHILIA YA MFALME EDIPODE KAMA KAZI YA UHALISIAJABUen_US
dc.typeThesisen_US


Files in this item

Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record