Athari za matamshi ya Kinyankore katika ujifunzaji wa lugha ya Kiswahili katika shule za upili wilayani Ntungamo, kusini -magharibi mwa Uganda
Abstract
Malengo ya Utafiti. Lengo Kuu: Lengo kuu la utafiti huu lilikuwa ni kuchanganua athari za matamshi ya Kinyankore katika ujifunzaji wa lugha ya Kiswahili katika shule za upili wilayani Ntungamo, Kusini-Magharibi mwa Uganda. Malengo Mahususi. Utafiti huu ulikuwa na malengo mahususi mawili: (i) Kuchunguza athari za lugha ya Kinyankore katika matamshi ya vitenzi vya Kiswahili. (ii) Kubainisha athari za lugha ya Kinyankore katika matamshi ya nomino za Kiswahili.