Athari ya lafudhi ya kikamba katika kujifunza matamshi ya Kiswahili
Abstract
Swala la matamshi ya lugha limezua mjadala pale ambapo wanafunzi wengi wanaopata shida ya matamshi ya Kiswahili ni kwamba wanatumia zaidi lugha mama ya kikamba shuleni katika kufanya mawasiliano badala ya kutumia lugha ya Kiswahili. Hii inawawia vigumu kutumia lugha ya Kiswahili na vilevile kuwa vigumu kwa walimu kufundisha lugha ya Kiswahili darasani. Baadhi ya misamiati ya lugha ya Kiswahili katika lugha ya kikamba na athari ya kimatamshi zinazotokana na ndimi za wahusika kuathiriwa na lugha mama na kusababisha kukosekana kwa baadhi ya sauti kama /d/, /r/, /t/, /n/, /b/. Pale ambapo mtu ambaye ameathiriwa na lafudhi ya Kikamba badala ya kusema 'kuja' yeye husema 'kunja', pia badala ya kusema 'bado' yeye husema 'bando', 'chakura' badala ya kusema 'chakula'. Hivyo basi, unapata mtu anaongea lugha potovu na hatimaye muda mwingine kuchanganya maana ya kitu fulani. Mbunda (1996 anasema kujifunza Kiswahili ambayo ni lugha ya pili kwa watanzania wengi ni ngumu; wanafunzi wa makabila wanashindwa kumudu Kiswahili kutokana na athari za lugha mama). Kwa hivyo, kulingana na mimi namuunga mkono Mbunda (1996) kwasababu nchini Kenya wanafunzi wa makabila wanashindwa kumudu Kiswahili kutokana na athari za lugha mama hasa wakamba ambao ndimi zao zinawaathiri na kusababisha kukosekana kwa baadhi ya sauti za Kiswahili.