Ulinganishaji wa uundaji nomino za lugha ya Kiswahili na lugha ya Runyankole kutoka vitenzi
Abstract
Kwanza kabisa, ninapenda kumshukuru mwenyezi Mungu mwingi wa rehema ambaye amenisaidia na
amenibariki katika kufanikisha kazi yangu hii. Shukurani zangu za pekee zimwendee msimamizi wangu
wa utafiti huu Dktr. Masengo innocent kwa kubeba jukumu la kuisimamia vyema kazi hii.
Nimemshukuru kwa ujasiri na uvumilivu wake mkubwa tokea hatua ya kuandika pendekezo la
utafiti hadi kumalizika kwa kazi hii. Ninaamini kuwa amenivumilia vya kutosha kwa udhaifu wangu
kama binadamu na kama mwanafunzi Mafanikio yaTasnifu hii yametokana na juhudi yake kubwa ya
kusoma, kukosoa , kurekebisha, kuelekeza na kushauri yale yote yanayofaa kuzingatiwa katika
utafiti huu. Licha ya majukumu mengi aliyonayo hakusita hata mara moja kusoma kazi yangu kwa
umakini mkubwa kwa wakati na kutoa maelekezo yanayojenga kazi hii kwa muda wote na wakati
ufaao. Sina cha kumlipa ila nina muombea ubariki kwa mwenyezi Mungu ampe maisha marefu
na amzidishie nguvu na imani ili aweze kutoa mchango kwa wanataaluma na taifa kwa ujumla.
Nawashukuru wahadhiri wote wa Idara ya Kiswahili katika Chuo Kikuu cha makerere kwa mchango
wao walionipa: BW.Wambette,Bw.Kyomuhendo victor,Dktr.masereka levi Mungu awape maisha
marefu na ya furaha katika maisha yao yote ili waendelee kutoa mchango wa kitaaluma na wa
kijamii katika Taifa letu. Vile vile ninatoa shukurani zangu za dhati kwa wanafunzi wenzangu wote
wa shahada ya uzamili ya Kiswahili wa mwaka wa masomo 2015/2019. Shukurani hizi za pekee
zimetokana na ushirikiano wao wa dhati kwa kipindi chote cha masomo ya uzamili. Mwenyezi
Mungu awazidishie moyo wa kupendana na kusaidiana. Vilevile, ninatoa shukurani zangu za dhati
kwa wazazi wangu, mzee mugume zepha na nakate sedridah pamoja na familia yangu kwa
kuniendeleza kielimu hadi kufikia hatua hii ya juu. Nawashukuru kwa msaada wao wa hali na
mali, Mwenyezi Mungu awajalie afya na rehema tele.