Show simple item record

dc.contributor.authorNankunda, Catheline
dc.date.accessioned2021-03-23T12:26:12Z
dc.date.available2021-03-23T12:26:12Z
dc.date.issued2021-03-11
dc.identifier.citationNankunda C., (2021 Athari za itikadi katika tamthilia ya mfalme edipode na kinjikitile. Unpublished undergraduate dissertation. Makerere University, Kampala-Ugandaen_US
dc.identifier.urihttp://hdl.handle.net/20.500.12281/9760
dc.descriptionA research project submitted in partial fulfillment of the requirements for the award of the degree of bachelor of Arts with Education of Makerere University.en_US
dc.description.abstractUtafiti huu unahusu Athari za itikadi katika tamthilia ya mfalme Edipode na Kinjikitile. Lengo kuu la utafiti huu ni kuchunguza athari za itikadi katika tamthilia ya mfalme Edipode na Kinjikitile . Malengo mahususi ni kubainisha itikadi zinazojitokeza katika tamthilia ya mfalme Edipode, kubainisha mbinu za kisanaa zilizotumika kuibua itikadi katika tamthilia ya mfalme Edipode na Kinjikitile na kulinganisha na kulinganua suala la itikadi katika tamthilia ya mfalme Edipode na Kinjikitile. Ili kukamilisha malengo haya, data za utafiti zilikusanywa kwa kutumia mbinu za usomaji wa machapisho , hojaji na mahojiano. Utafiti huu umetumia nadharia mbili yaani nadharia ya umarx na nadharia ya kimaadili. Matokeo ya utafiti yanaonyesha kuwa itikadi kama vile dini, maadili, utawala na utamaduni zimejitokeza katika tamthilia ya mfalme Edipode. Kwa upande wa kinjikitile ,tumebainisha itikadi za uzazi na malezi, utawala, mapinduzi, dini, ubepari na ujamaa .Matokeo ya utafiti huu yanaonesha kwamba kila itikadi inakuwa na athari yake kwa jamii hasa ile ya dini imetawala maisha ya watu wengi wa ulimwengu na jambo hili linathibitisha kuwa kwa asili, mwanadamu ni mtu ambaye anazaliwa akiwa na itikadi ya uwepo wa Mungu. Pia, matokeo ya utafiti huu yanaonesha kuwa itikadi katika tamthilia teule zinajegwa kwa kutumia maudhui na wahusika ambao mtafiti anawatumia kuwasilisha athari za itikadi katika tamthilia teule. Kwa hivyo, tunahitimisha kwamba itikadi nyingi ambazo zinajitokeza katika tamthilia ya Mfalme Edipode na Kinjikitile zinahusiana na maisha ya kila siku ya watu wa jamii na itikadi hizo ndizo zinazoongoza maisha ya kila siku ya jamii hizo kwa mfano dini. Mwishoni tunapendeza utafiti kama huu ufanywe katika vitabu vingine vya tanzia vya sasa na vya kijadi ili kulinganisha na kulinganua namna suala la itikadi linavyojitokeza na namna linavyobadilika badilika kadri muda unavyosonga.en_US
dc.language.isootheren_US
dc.publisherMakerere University.en_US
dc.titleAthari za itikadi katika tamthilia ya mfalme edipode na kinjikitile.en_US
dc.typeThesisen_US


Files in this item

Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record