Usawiri wa mwanamke katika tamthilia ya kilio cha haki na chema chajiuza.
Abstract
Andiko hili la mradi linalenga kuchunguza usawiri wa mwanamke katika tamthilia ya Kilio cha Haki na Chema Chajiuza. Mradi huu unalenga kugundua namna wanawake wanavyochukuliwa katika tamthilia hizo mbili kwa sababu muda ambao zimepishana ni
mwingi sana yaani Kilio cha Haki (1981) na Chema Chajiuza (2018). Lengo la mradi huu limeshughulikiwa ipasavyo baada ya kukusanya data za mradi kwa kutumia mbinu za usomaji makini na upitiaji wa nyaraka. Matokeo ya mradi yamebainishwa kuwa mwanamke amesawiriwa kwa nafasi mbili yaani chanya na hasi kama vile; mlezi, mfanya kazi na bidii Jasiri, mtiifu, mwadilifu, mvumilivu, mwoga, chombo cha kustarehesha mwanamume na kadhalik