Matumizi ya mbinu za sanaa katika ngano za lugha ya Kiswahili na lugha ya Kinyankole
Abstract
Sura ya kwanza ilijihusisha na usuli wa mada, suala la utafiti, madhumuni ya utafiti, upeo wa utafiti na changamoto zitakazomkumba mtafiti. Mbinu za sanaa ni ubunifu wa kisanaa unaojitokeza baada ya kusoma au kusikiliza masimulizi. Angalau unapaswa kusoma sentensi kadhaa au hata hadithi nzima ili kutambua mbinu ya sanaa iliyotumika.
Kwa mjibu wa Senkoro (2011), ngano ni utanzu wa fasihi simulizi ambao ulipitishwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine kwa njia yamdomo. Kwa hivyo mtafiti atashughulikia angalau ngano kumi na mbili tofauti za lugha ya Kiswahili na Kinyankole.