Kulinganisha Maudhui ya ukoloni katika tamthilia ya Mzalendo Kimathi na Kilio Cha Haki
Abstract
Tamthilia ni utanzu wa fasihi ambao huwasilisha ujumbe wake kwa njia ya usimulizi ama
kimaandishi. Kwa mujibu wa Wamitila (2007), huu ni utanzu ambao huandikwa kwa
mtindo wa mazugumzo ya wahusika. Tamthlia ambazo tuliteua zilibeba maudhui ya
ukoloni ndani yaani Mzalendo Kimathi na Kilio Cha Haki.
Aidha, Wamitila anasema kwamba maudhui ni jumla ya mambo yote yanayozungmziwa
katika kazi ya kifasihi. Katika utafiti huu tutachunguza maudhui ya utawala ya kikoloni
kwa kulinganisha tamthiliya ya Mzalendo Kimathi na ya Kilio cha Haki ili kugundua
usawili wa ukoloni katika kazi hizi za Fasihi.
Fasihi ni sanaa inayotumia lugha bunifu ili kueleza tajriba mbalimbali za maisha ya
wanajamii. Njogu na Chimerah (1999) wanaeleza kuwa fasihi inawasilisha hali,
mwingiliano, mivutano na mikinzano miongoni mwa binadamu na mazingira yake.
Utafiti huu unahusu ulinganishaji wa maudhui ya utawala ya Kikoloni katika tamthilia
mbili za Kiswahili. Hapa tunachunguza jinsi waandishi wa tamthilia walivyosawiri
maudhui ya ukoloni katika kazi zao za fasihi.